1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Makubaliano kuhusu wafungwa yafikiwa kati ya Israel na Palestina

1 Januari 2007

Makubaliano ya kubadilishana wafungwa yamefikiwa kati ya Israel na Palestina katika juhudi ya kuachiliwa huru kwa mwanajeshi wa Israel anayezuiliwa na wanamgambo wa kipalestina.

Duru nchini Palestina zimearifu kuwa mpango huo utakaoruhusu wafungwa wa kipalestina wanaozuiliwa na Israel kuachiliwa huru, utatangazwa Alhamisi ijayo kwenye mkutano kati ya rais wa Misri, Hosni Mubarak, na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert.

Misri imekuwa mpatanishi mkuu katika mazungumzo baina ya makundi ya Israel na Palestina kuhusiana na kuachiliwa huru wafungwa wa kipalestina na mwanajeshi wa Israel, koplo Gilad Shalit.

Shalit alitekwa nyara na wanamgambo wa kipalestina mnamo mwezi Juni mwaka jana mjini Gaza, hatua iliyosababisha uvamizi wa jeshi la Israel ambapo mamia ya wapalestina waliuwawa.

Waziri Olmert amezungumza kwa njia ya simu na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa wa kipalestina kutoka jela za Israel