GAZA: Mashambulio ya Israel yaendelea
9 Julai 2006Matangazo
Si chini ya Wapalestina 2 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa katika mashambulio yaliyofanywa na vikosi vya anga vya Israeli katika Ukanda wa Gaza.Walioshuhudia mashambulio hayo wamesema kuwa miongoni mwa waliokufa ni mtoto wa kike aliekuwa na umri wa miaka 6.Hapo awali,waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert alikataa mwito wa kukomesha mapigano uliotolewa na waziri mkuu wa Wapalestina Ismail Haniyeh.Olmert amesema,mapigano hayatosita mpaka wanamgambo wa Kipalestina watakapomuachilia huru,mwanajeshi wa Kiisraeli Gilad Shalit aliyetekwa nyara wiki mbili za nyuma.Wakati huo huo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada na huduma za kiutu katika Ukanda wa Gaza,John Ging,amesema hali katika eneo hilo ni janga kubwa la kiutu.
