1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mkutano wa viongozi wa Israil na Palestina waahirishwa.

7 Juni 2007

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amefutilia mbali mkutano uliopangwa kati yake na Waziri Mkuu wa Israil Ehud Olmert.

Rais Mahmoud Abbas amechukua hatua hiyo akitaka kuhakikishiwa na Israil kwamba itawawasilishia Wapalestina fedha inazozizuia miongoni mwa hatua nyingine kabla ya mashauriano hayo kuendelea.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili ulipangwa kuwa leo katika mji wa Jericho kwa lengo la kufufua mashauriano ya amani yaliyokwama yaliyokuwa yamesimamiwa na Marekani.

Mashauriano hayo yamekwama tangu mwezi Aprili.

Marekani haijazingatia sana hatua hiyo ya kuahirishwa mkutano huo na imesema pande zinazohusika zimejitolea kidhati kuhakikisha kuwepo amani Mashariki ya Kati.