1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mkuu wa makachero nchini Misri akutana na rais Abbas wa Palestina

29 Agosti 2005

Mkuu wa makachero nchini Misri, Omar Suleiman, amekutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas leo kujadili njia ya kuendeleza kusitishwa kwa mapigano na kuwepo kwa vituo vya mpakani katika ukanda wa Gaza baada ya Israel kuondoka eneo hilo.

Ziara ya Omar inafanyika siku moja tu baada ya shambulio la mpalestina wa kujitoa muhanga na ni juhudi za kuwahimiza wanamgambo kukomesha machafuko, hususan kabla kuondoka kwa wanajeshi wote wa Israel kutoka Gaza katikati ya mwezi ujao.

Waziri mkuu wa Palestina, Ahmed Qurei amewaambia waandishi habari kwamba makubaliano yataafikiwa juu ya kituo cha Rafah kati ya Gaza na Misri. Amesisitiza kwamba wapalestina wanataka kituo hicho kiwe mikononi mwa Misri na Palestina.