UNICEF yasema Gaza ni hatari kwa watoto
23 Novemba 2023Matangazo
Aidha amengeza kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas hayatoshi kuyaokoa maisha yao.Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Catherine Russell ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa zaidi ya watoto 5,000 wameripotiwa kuuawa huko Gaza tangu shambulizi la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7, hiyo ikiwa ni asilimia 40 ya vifo mpaka sasa.Russell amesema ili watoto waishi na wafanyakazi wa kibinaadamu wabaki eneo hilo na kufanya kazi yao kwa ufanisi, mipango ya kusitisha vita kwa nyakati fulani ili kuruhusu huduma za kiutu haijitoshelezi.