1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Palestina yasisitiza majadiliano kumpata mwanajeshi aliyekamatwa wa Israel.

29 Julai 2006

Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh , amesema kuwa njia pekee ambayo Israel inaweza kumpata mwanajeshi wake aliyetekwa na tawi la kijeshi la chama cha Hamas mwezi uliopita ni kwa njia ya majadiliano.

Akizungumza katika msikiti mmoja mjini Gaza wakati wa swala ya Ijumaa, Haniyeh amerejea wito wa Wapalestina wa kufanyika hatua za kisiasa na kidiplomasia ili kuweza kupata kuachiwa kwa mwanajeshi huyo, ambaye alitekwa nyara kutoka Israel na Wapalestina wenye silaha mwishoni mwa mwezi wa Juni.

Hamas inataka kuachiliwa huru kwa wafungwa 10,000 wa Kipalestina kwa kubadilishana na mwanajeshi huyo mmoja. Israel imekataa madai hayo.