GAZA: Shambulio la Israel limelenga wanamgambo wa Hamas
19 Novemba 2006Matangazo
Ripoti kutoka Gaza zinasema,shambulio la angani la Israel lililolenga gari la mwanamgambo wa Kipalestina limewajeruhi watu wasiohusika. Wanachama wawili wa Hamas waliokuwa ndani ya gari lililolengwa,walijeruhiwa lakini waliweza kujiokoa dakika ya mwisho.