1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA Viongozi wa Palestina na Israel kukutana kwa mazungumzo juu ya usalama

23 Mei 2005

Waziri wa Ulinzi wa Israel Shaul Mofaz na waziri wa mambo ya ndani wa Palestina Nasr Yussuf jioni hii wanatarajiwa kukutana kwa mazungumzo juu ya usalama.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Palestina,amesema viongozi hao wawili wamejipanga kuzungumzia juu ya mpango wa Israel ulioshindwa, wa kuwarejeshea wapalestina madaraka ya usalama katika miji ya magharibi mwa ukingo wa ghaza pamoja na mzozo uliozuka hivi karibuni katika eneo la ukanda wa gaza. Wakati huo huo wanadiplomasia wamesema,katika ziara yake ya kwanza wiki hii kwenye ikulu ya Marekani ,rais wa Palestina Mahmoud Abbas anatarajiwa kumtaka rais Bush kuisisitiza Israel kuutekeleza mpango wa amani wa Road Map.

Israel iliusimamisha mpango wa kuwarejeshea wapalestina miji yao mitatu ya magharibi mwa ukingo wa ghaza mapema mwezi huu kufuatia mpango mwengine kama huo wa kuirejesha miji ya Jericho na Tulkarem huku ikishutumu Palestina kwa kutofanya vya kutosha kuyavunja makundi ya wanamgambo.

Mashambulio ya vifaru katika eneo la ukanda wa ghaza wiki iliyopita kumerejesha hali ya wasiwasi juu ya makubaliano ya amani ya mashariki ya kati, tangu wanamgambo wa kipalestina walipokubali kuacha mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Israel mwezi hapo mwezi Januari.