GAZA: Wajumbe wa Hamas na Fatah kukutana Misri
25 Mei 2007Matangazo
Wajumbe wa makundi hasimu ya Kipalestina,Hamas na Fatah wanatarajiwa kwenda Cairo hivi karibuni. Wajumbe hao,chini ya usimamizi wa Misri,hasa watashughulikia matatizo ya ndani ya Wapalestina,lakini hata suala la kukubaliana na Israel kuweka chini silaha litazungumzwa.Maafisa wa Hamas na Fatah watakuwa na majadiliano mbali mbali na wapatanishi wa Kimisri.Ujumbe wa Fatah wenye watu 6 hiyo kesho utakwenda Cairo kwa majadiliano ya siku tatu.Mohammed Dahlan alie mshauri wa Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas, kuhusu masuala ya usalama wa taifa,ameshawasili Cairo.