1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA Wanadiplomasia wa umoja wa Ulaya wakutana na viongozi wa Palestina

16 Juni 2005

Wanamgambo wa kundi la Hamas katika mkanda wa Gaza, wamefichua kwamba wanadiplomasia wa umoja wa Ulaya walikutana na baadhi ya wanachama wake. Hatua hiyo mpya ya maongozi ya umoja huo, imekosolewa vikali na Israel.

Wakati huo huo, makombora mawili yamevurumishwa na wanamgambo hao kutoka eneo la kazkazini mwa mkanda wa Gaza na kuanguka katika mji wa Sderot, kusini mwa Israel. Makombora hayo aina ya Qassam yalaianguka katika kiwanja cha chuo kimoja mjini humo. Duru za jeshi la Israel zinasema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW