1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wanamgambo wa kipalestina wamteka nyara ripota wa Marekani na mpiga picha wa Uingereza huko Gaza

13 Oktoba 2005

Wanamgambo wa kipalestina waliwateka nyara na kuwazuia kwa mda mfupi ripota wa Marekani, Dion Nissenbaum na mpiga picha wa Uingereza, Adam Pletts, katika ukanda wa Gaza. Tukio hilo la hivi punde linadhihirisha kuzorota kwa usalama katika eneo hilo, na kibarua kinachomkabili rais Mahmoud Abbas katika kudumisha utulivu, baada ya Israel kuondoka Gaza.

Wanaume hao wawili wanaofanya kazi na gazeti la Knight Riddler walitekwa nyara karibu na mji wa Khan Younis. Baada ya saa saba waliachiliwa huru kufuatia mazungumzo kati ya maofisa wa Palestina na watekaji nyara hao, wa kundi la Black Panther, kikundi kilichojitenga kutoka kwa kundi la Fatah.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW