1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:

18 Agosti 2005

Wanajeshi wa Israel mapema leo wameingia katika makazi ya walowezi wa Kiyahudu huko Gan Or,katika ukanda wa Gaza,wakiwa wanaendelea na operesheni yao ya kuwaondoa kwa nguvu walowezi wakaidi waliong’ang’ania katika maeneo yao.

Askari polisi wa Israel waliingia kwa nguvu katika lango la wanajumuia ya walowezi hao na kukabiliana na kikundi cha wasichana waliokuwa wanajaribu kuwazuia kuingia katika makazi yao,lakini hata hivyo hawakuweza kufua dafu mbele ya askari hao.

Kiasi cha watu 350 wanaishi eneo hilo la Gan Or.

Hadi sasa wanajeshi wa Israel wamefanikiwa kuyahamisha makazi ya walowezi wa Kiyahudi 11 kati ya 21 eneo la Gaza,tangu operesheni ya kuwahamisha walowezi hao kwa nguvu ilipoanza jana.

Katika tukio jingine mlowezi mmoja wa Kiyahudi aliwauwa wafanyakazi wanne wa Kipalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi,baada ya kufanikiwa kumpokonya bunduki mlinzi mmoja.Baada ya tukio hilo wanamgambo wa Kipalestina walilipiza kisasi kwa kuvurumisha maroketi mawili kuelekea makazi ya Walowezi wa Kiyahudi.Hata hivyo hakujatolewa taarifa yoyote ya majeruhi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW