1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza.Majeshi ya Israel yawauwa wanamgambo wawili wa Hamas.

31 Oktoba 2006

Vikosi vya kijeshi vya Israel vimewauwa wanamgambo wawili wa Hamas katika Ukanda wa Gaza kufuatia mapigano kati ya Wapalestina waliokuwa na silaha na wanajeshi wa Israel.

Msemaji wa jeshi amesema mashambulizi hayo yamekuja kufuatia msako unaoendelea dhidi ya wanamgambo katika maeneo ya karibu na mji wa Khan Younis.

Jeshi la Israel limesema kuwa lilianzisha operesheni hiyo katika mamlaka ya Wapalestina ili kuwazuia wanamgambo wasirushe maroketi nchini Israel.

Israel imeshawauwa wapalestina zaidi ya 250 nusu yao wakiwa ni raia wa kawaida kufuatia hujuma zake huko Gaza, ambazo zilianza mara tu baada ya watu wenye silaha kutoka katika mamlaka ya Wapalestina kumteka mwanajeshi wake mnamo mwezi June.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW