1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Waandamanaji wavamia afisi za umoja wa mataifa

31 Julai 2006

Waandamanaji wenye hasira walivamia afisi za umoja wa mataifa nchini Palestina na kufanya uharibifu katika afisi hizo sambamba na waandamanaji katika mji wa Beirut nchini Lebanon waliovamia afisi za umoja wa mataifa na kufanya uharibifu katika hatua ya kupinga mauaji ya raia yaliyofanya na majeshi ya Israel katika mji wa Qana nchini Lebanon.

Maafisa wa usalama walilazimika kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji hao katika mji wa Gaza.

Wakati huo huo ndege za jeshi la Israel zimeyashambulia makaazi mawili ya wapiganaji wa Hamas na kuwajeruhi watu wawili kwa mujibu wa habari kutoka Palestina.

Israel imekiri kuwa ndege zake zimeshambulia jumba linalokaliwa na wapiganaji wa kipalestina wenye msimamo mkali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW