Gazeti la kila siku la TAGESSPIEGEL kutoka Berlin linauchambua mkutano wa chama-tawala cha SPD unaofanyika leo mjini Berlin likiandika:
31 Agosti 2005Gazeti la kila siku la TAGESSPIEGEL kutoka Berlin linauchambua mkutano wa chama-tawala cha SPD unaofanyika leo mjini Berlin likiandika:
“Matokeo ya uchaguzi mkuu yatafuta kile ambacho wajumbe wa mkutano wa leo wataamua:yaani kitu cha kujivunia kipindi cha utawala cha serikali ya muungano kati ya chama cha SPD na cha walinzi wa mazingira cha KIJANI na ujasiri wake wa kupitisha mageuzi ambayo licha ya upinzani chamani ,haikurudi nyuma.Baada ya hapo hatima ya serikali hiyo itapitishwa na Kanzela mpya atakua hasa Bibi Angela Merkel…. Pamoja na kuacha madaraka kwa mawaziri wote waliochangia mageuzi hayo.Hakutakua na mkumbo wa upinzani wa kutetea amani na mazingira safi kama ilivyokua 1982,bali mkumbo huu utakumbana na mashindano ya kundi jengine la mrengo wa shoto Bungeni.”
Gazeti la NEUE PRESSE kutoka Hannover, linahisi chama cha SPD kina ukosefu wa wanasiasa wa kutosha wa kukitembeza chama kwa wapiga kura:
Laandika kwamba, chama cha upinzani cha CDU kina Bw.Kirchohof na von Pierer-yaani vigogo ambavyo vinaweza kuchangia barabara mjadala huo na kutegemea kuungwamkono na wanaviwanda. Wote wawili wanakitia jeki chama cha upinzani katika awamu hii ya mwisho kuelekea uchaguzi.
Na chama cha SPD kina nani ? Kina Gerhard Schröder tu na si mwengine-Schröder,Schröder anaehanikiza kila mahala.Nyuma yake hakuna wengine wengi.Hiki ni chama kinachosaka binafsi kilikoelemea.Ni maoni ya NEUE PRESSE:
Ama gazeti la FINANCIAL TIMES LA UJERUMANI laandika:
“Kampeni ya uchaguzi ya chama-tyawala cha SPD ina mambo ya kutatanisha yanayofahamika na ambayo hata chamani yanatambulika.Kosa halipo katika ukosefu wa maandalio,bali katika ukosefu wa njia za kufuata.Yule anaeona ukweli, basi anajua kwamba Schröder,hataweza kukipatia chama ushindi.Isipokua chama hakimudu kusema hivyo ili kutombomoa Kanzela wake au kujichimbia binafsi kaburi…..” ni maoni ya FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND.
Likitugeuzia mada –kupanda mno kwa bei ya ma futa kunaangaliwa na gameti la HEILBRONNER STIMME kama ni hatari kubwa katika kuufufua uchumi wa Ujerumani.Laandika:
“shinikizo linalotikisa uchumi wa Ujerumani linazidi kuongezeka.Bado mageuzi yalioanzishwa yanaweka tumaini zaidi la kupambazuka hali ya mambo hasa baada ya uchaguzi ujao,lakini hii haitadumu muda mrefu.
Gharama kubwa za kununulia mafuta ya petroli zitaathiri pia hali hii dhaifu ya kustawi upya uchumi.Njia ya kujikomboa kutoka ni kuondoa kodi ya kimazingira.Kufanya hivyo, kutaleta mzigo kwa muda mfupi katika mfuko wa bima ya wastaafu,lakini ishara itakayotoa itachangamsha soko la ndani na hii itasawazisha athari iliozuka.”
Hata mada ya kuzuwia kuchafuka hali ya hewa kwa jicho la kimbunga “Patarina” kilichopiga Marekani,kimechambuliwa na wahariri:
Gazeti la RHEIN-ZEITUNG lionalotoka KOMBLENZ laandika:
„Kwa muda gani zaidi tuvumilie kutochukuliwa hatua na tukitumbua macho tu misiba ya kimaumbile inateketeza kile binadamu wamekijenga kwa karne kadhaa ? Kwa kuwa na viwanda vikubwa na kuzidi idadi ya watu duniani,matumizi ya sayari hii mnamo karne ya 19 yameingia katika daraja ambayo raslimali ziliopo duniani zimeanza kuathirika.Kwahivyo, tungojee hadi lini,mpaka tuzindukane na kubadili vitendo vyetu na kuelekea upande mwengine ?