1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

The Moscow Times yaorodheshwa kama wakala wa kigeni

18 Novemba 2023

Wizara ya sheria ya Urusi jana ililiongeza gazeti la mtandaoni la The Moscow Times lenye umaarufu miongoni mwa jamii ya wataalamu wa Urusi walioko nje ya nchi hiyo kwenye orodha yake ya mawakala wa kigeni

Raia wa Urusi wakisoma magazeti ya nchi hiyo
Raia wa Urusi wakisoma magazeti ya nchi hiyoPicha: Peter Kovalev/TASS/picture alliance/dpa

Wizara ya sheria ya Urusi jana ililiongeza gazeti la mtandaoni la The Moscow Times lenye umaarufu miongoni mwa jamii ya wataalamu wa Urusi kwenye orodha yake ya mawakala wa kigeni. Hatua hiyo ni muendelezo wa msako mkali unaoendeshwa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya vyombo vya habari vinavyoikosoa pamoja na vyama vya upinzani.

Athari ya kuorodheshwa kama wakala wa kigeni

Jina la mawakala wa kigeni, huwaweka watu binafsi na mashirika chini ya uchunguzi mkali wa kifedha na huhitaji taarifa zao zijumuishe notisi ya kueleza kuwa wametajwa kuwa mawakala wa kigeni. 

Kutajwa kwa watu binafsi na mashirika kuwa mawakala wa kigeni, kunaonekana kama udhalilishaji unaolenga kuhujumu uadilifu wa walioorodheshwa.
 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW