1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gbagbo angángánia madaraka Cote d´Ivoire

7 Aprili 2011

Vikosi vinavyomuunga mkono Alassane Ouatarra, anaetambuliwa kimataifa rais wa Cote d´Ivoire, bado havikufanikiwa kumkamata Laurent Gbagbo aliejificha katika handaki, ndani ya Ikulu yake mjini Abidjan.

Soldiers loyal to democratically elected president Alassane Ouattara return from fighting to a checkpoint serving as an operating base, at one of the main entrances to Abidjan, Ivory Coast, Wednesday, April 6, 2011. Heavy arms fire rang out Wednesday near the home of the country's strongman who remained holed up in a subterranean bunker, as forces backing his rival assaulted the residence to try to force him out, diplomats and witnesses said. (AP Photo/Rebecca Blackwell)
Vikosi vya Alassane Ouatarra vimepania kumkamata Laurent GbagboPicha: AP

Vikosi hivyo vimekabiliwa na mapigano makali kutoka wafuasi wa mwisho wa Gbagbo, anaepinga kabisa kuondoka madarakani, licha ya jeshi lake kusalim amri Jumanne iliyopita.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa, majadiliano yanafanywa pamoja na Gbagbo lakini kiongozi huyo binafasi ameiambia stesheni moja ya redio ya Ufaransa kuwa hana azma ya kuondoka madarakani.

Raia wakimbia mapigano makali katikati ya mji mkuu AbidjanPicha: Picture-alliance/dpa

Umoja wa Ulaya unamlaumu Gbagbo kusababisha umwagaji damu huu mpya na umeweka vikwazo vipya dhidi ya Gbagbo, kwa kupiga marufuku kununua hisa za serikali yake. Umoja wa Ulaya umeshaweka vikwazo kadhaa dhidi ya Gbagbo na washirika wake, baada ya kiongozi huyo kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi wa Novemba mwaka jana na kuondoka madarakani kufuatia.