Gbagbo kushawishiwa aondoke!
28 Desemba 2010Ujumbe wa viongozi wa nchi za jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS unatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan leo ili kujaribu kumshawishi rais Laurent Gbagbo aondoke madarakani. Ujumbe huo ni wa viongozi kutoka,Benin,Sierra Leone na Cape Verde Jumuiya ya Ecowas imetishia kutumia nguvu ili kumwondoa Gbagbo madarakani ikiwa rais huyo atakataa kuondoka kwa hiari yake.
Wakati huo huo taarifa kutoka Abidjan zinesema wafanyakazi wengi wa mji huo waliupuuza mwito wa kushikiri katika mgomo wa nchi nzima uliotolewa na kiongozi wa upinzani Alassane Outtara anaetambuliwa kuwa mshindi wa uchaguzi .Vyombo vya habari vimearifu kuwa kazi ziliendelea kama kawaida kwenye bandari muhimu za Abidjan na San Pedro zinazotumika kusafirishia zao muhimu la kakao.Maduka yalifunguliwa na watu walienda ofisini.