1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gebrie Selassie wa Ethiopia,ashinda Berlin Marathon

Ramadhan Ali25 Septemba 2006

Muethiopia Haile Gebreselassie, alishinda jana mbio za Berlin marathon kwa muda bora msimu huu .Katika upande wa wanawake,ushindi pia ulikwenda Ethiopia:Gete Wami alitamba.

Gete Wami baada ya kushinda Berlin marathon
Gete Wami baada ya kushinda Berlin marathonPicha: AP

Tukianza na Ligi mashuhuri barani Ulaya, sehemu kubwa ya timu maarufu za Ulaya, zinazorudi kesho uwanjani kwa champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya, zilitumia changamoto za mwishoni mwa wiki kwa maandalio ya Kombe hilo:Bayern Munich,mabingwa wa Ujerumani, wamerudi kileleni.Chelsea,Arsenal na Liverpool zilitamba pia nyumbani sawa na Real Madrid .Mahasimu wao na mabingwa watertezi FC Barcelona walizimwa na Valencia na kubidi kuridhika na suluhu ya bao 1:1.

Mabingwa Bayern Munich walitoka nyuma na kuichapa Alemania Aachen mabao 2:1 na kuparamia tena kileleni mwa Bundesliga.Ijumaa iliopita Borussia Mönchengladbach iliipiga teke Berlin kutoka kileleni na kukikalia binafsi kilele hicho hadi pale jana Nuremberg ilipozimwa na Energie Cottbus na kupoteza pointi 2 ilizohitaji kurudi kileleni mwa Ligi.Waakilishi wengine wa Ujerumani kutoka bundesliga –hamburg na Bremen, waliachana suluhu bao 1:1 .

Ama katika Premier League, Ligi ya Uingereza, mabingwa Chelsea wameparamia kileleni kwa mara ya kwanza tangu kuanza msimu huu.Chelsea iliizaba Fulham mabao 2:0.Arsenal,makamo-bingwa waliitandika Sheffield mabao 3:0.Manchester united walimudu sare tu 1:1 dhidi ya Reading.Portsmouth iliowasangaza wengi msimu huu ilipoanza kwa kasi,yaweza kuipiku Chelsea kileleni leo wakiwika mbele ya Bolton Wandereres.

Huko Itali,Inter Milan ilipanda kkleleni jana walipoilaza Chievo Verona mabao 4-3 huko San Siro.

Olympique Lyon ya Ufaransa,imeendelea kupiga makasia kuelekea kunyakua taji lao la 6 baada ya kuizaba Lille mabao 4:1.

Katika La Liga-Ligi ya Spain, mabingwa Fc Barcelona waliteleza kidogo walipomudu suluhu bao 1:1 kati yao na Valencia.Real Madrid lakini ndio ilioparamia kileleni ilipoichapa Real Betis bao 1:0.

Kombe la CEC AFA la chipukizi chini ya umri wa miaka 20 lilinyakuliwa jana na Uganda kufuatia finali ya kusisimua mjini Bujumbura kati yake na Burundi.Bakari Ubena anasema-

Bingwa mara 2 wa olimpik wa masafa ya mita 10.000,Haile Gebreselassie wa Ethiopia,alishinda jana mashindano ya 33 ya Berlin marathon wakati mwenzake wa kike Gete Wami,alitamba upande huo.

Gebreselassie alichukua muda wa masaa 2 dakika 5 na sek.56 na hivyo ameufuta muda bora kabisa wa masafa haya kwa mwaka huu.Alishindwa lakini kuivunja rekodi ya dunia ya mkenya Paul Tergat alioiweka Septemba mwaka 2003 ya masaa 2, dakika 4 na sek.55.

Gudisa Shentema alimaliza wapili huku Mjapan Kurao Umeki.Wakenya 3 walichukua nafasi ya 7,8 na 9.Ombeche Mokamba alikuja wa 6,Jackson Koech 8 na Abel Kirui alikuja wa 9.Buzinggo Donatien kutoka Burundi alitokea 10.

Ama upande wa wanawake, Gete Wami wa Ethiopia alinyakua ushindi kwa muda wake wa masaa 2:21:34.

Wapili alifuata mkenya Salina Kosgei na nafasi ya tatu ikaenda kwa Monika Drybulska wa Poland.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW