GENEVA: Azimio la Darfur lapitishwa
30 Machi 2007Matangazo
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio lililowasilishwa na mataifa ya Ulaya na Afrika yakielezea wasiwasi wao juu ya hali ya jimbo la Darfur nchini Sudan.
Aidha baraza hilo limesema litaendelea kuifuatilia kwa karibu hali katika eneo la Darfur.
Hata hivyo azimio hilo halikuikosoa serikali ya Sudan kwa jukumu lake katika ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la Darfur.
Makubaliano yalifikiwa baada ya Ujerumani kukubali kuondoa kifungu cha maneno kilichoeleza jukumu la serikali ya Khartoum katika mashambulio dhidi ya raia wa Darfur na uharibifu
wa vijiji.