1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Bado kuna utumwa duniani .

12 Mei 2005


Sera ya utandawazi na utashi wa nguvukazi za bei nafuu zimesabisha watu zaidi ya milioni 12 kutumikishwa kama watumwa katika sehemu mbali mbali za dunia.

Nusu ya watu hao ni watoto.

Shirika la kazi duniani ILO limesema kwamba idadi kubwa ya watu hao wapo barani Asia na Latin Amerika ambapo wengi wanatumikishwa mashambani ama katika kambi ambapo wanalazimishwa kufanya kazi.

Katika taarifa yake shirika hilo pia limesema hasa wanawake na watoto wapo katika hatari kubwa ya kunaswa katika mazingira kama hayo ambapo inakuwa vigumu kujinasua.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW