GENEVA: China na Urussi zapinga kujadili Darfur
17 Machi 2007Matangazo
China na Urussi zinapinga suala la mgogoro wa Darfur kujadiliwa katika mkutano wa Halmashauri ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva,nchini Uswissi.Mkutano huo unahusika na ripoti ya tume iliyoongozwa na Jody Williams alietunzwa zawadi ya amani ya Nobel.Tume hiyo ilinyimwa ruhusa ya kwenda katika jimbo la mgogoro la Darfur,magharibi ya Sudan.Kwa maoni ya wajumbe wa China na Urussi,suala la Darfur haliwezi kujadiliwa kwa sababu wajumbe waliotumwa na Halmshauri ya Haki za Binadamu hawakuweza kutekeleza ujumbe wao.Matamshi ya China na Urussi yanaiunga mkono serikali ya Sudan ambayo hapo awali tayari ilipinga ripoti ya tume hiyo.Katika ripoti hiyo,serikali ya Sudan imetuhumiwa uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.