GENEVA: Hakuna maafikiano kuzuia utapakaji wa silaha za kinuklia
28 Mei 2005Matangazo
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa,bwana Mohamed El-Baradei amesema,ni jambo linalosikitisha kuwa mkutano wa Umoja wa Mataifa,umeshindwa kuidhinisha hatua mpya za kupambana na utapakaji wa silaha za kinuklia.Ametoa muito pia kwa viongozi wa kimataifa kulitia maanani suala hilo.Amesema mkutano huo wa kuuchambua Mkataba wa kuzuia utapakaji wa silaha za kinyuklia uliokubaliwa mwaka 1970,umemalizika mjini New York kule ulipoanzia ukiwa na utaratibu uliojaa mianya.Madola 188 yaliohudhuria mkutano huo hayakuweza kukubaliana juu ya njia mpya za kuzuia utapakaji wa silaha za kinuklia.