GENEVA. Israel yakosolewa na tume ya haki za binadamu kwa kuyakalia maeneo ya Palestina.
15 Aprili 2005Matangazo
Tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa imelaani hatua ya Israel kuyakalia maeneo ya Palestina na kuitaka ibadili hatua hiyo. Azimio hilo lililopitishwa katika mkutano wa kila mwaka wa tume hiyo mjini Geneva, liliungwa mkono na mataifa 39. Marekani, na Australia ndiyo mataifa mawili pekee yaliolipinga azimio hilo, huku Ujerumani, Uingereza na Canada zikikosa kushiriki katika upigaji kura huo. Maazimio mengine mawili yanayoitaka Israel iondoke kutoka eneo la Golan na kulaani hatua ya Israel kutumia nguvu dhidi ya wapalestina, yalipitisha katika mkutano huo.