1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Lawama zatolewa kwa wizara ya ulinzi ya Marekani .

20 Mei 2005

Msemaji wa kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu amesema ,chama hicho kiliifahamisha wizara ya ulinzi ya Marekani kwamba mahabusi katika jela ya Gauntanamo waliripoti juu ya maafisa wa Marekani waliokuwa wanaikashifu Koran tukufu.

Msemaji huyo wa chama cha msalaba mwekundu ameeleza kwamba malalamiko ya wafungwa hao yaliwasilishwa mara kadhaa kwenye wizara ya ulinzi ya Marekani katika ya mwaka wa 2002 na mwaka 2003.

Suala la koran tukufu kukashifiwa na maafisa wa marekani katika jela ya Guantanamo liliripotiwa na gazeti la kila wiki la Marekani Newsweek hivi karibuni na kusababisha ghadhabu miongoni mwa waislamu katika eneo lote la mashariki ya kati.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW