GENEVA : Mazungunzo ya nuklea ya Iran na Umoja wa Ulaya kuendelea
26 Mei 2005Iran imekubali kuongeza muda wake wa kusitisha shughuli za kurutubisha uranium.
Hatua hii imekuja katika mkutano mjini Geneva Uswisi kati ya mkuu wa ujumbe wa usuluhishi wa Iran Hassan Rohani na ujumbe wa Umoja wa Ulaya unaoundwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jack Straw,waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Michel Barnier.Straw alizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo.
Rohani amesema anafikiri pande hizo mbili zinaweza kufikia makubaliano wa kile alichokiita muda mfupi ufaao.Iran inataka kuepuka kufikishwa kwa suala la mpango wake nuklea katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili uwezekano wa kuwekewa vikwazo.
Serikali ya Marekani inaishutumu Iran kutengeneza silaha za nuklea wakati Iran yenyewe inasisitiza kwamba mpango wake wa nuklea ni kwa ajili ya dhamira za amani.