1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Geneva: Mkataba wa plastiki washindwa kufikia makubaliano

15 Agosti 2025

Baada ya miaka mitatu ya mazungumzo ambapo nchi zipatazo 180 zilikuwa zinakubaliana kwamba takataka za plastiki ni kitisho kikubwa, lakini katika mkutano huo nchi hizo bado zimetofautiana katika masuala kadhaa.

Usiwsi I 2025 | Umoja wa Mataifa
Mazungumzo ya mkataba wa plastiki yashindwa kufikia makubaliano GenevaPicha: Tim Schauenberg/DW

Mazungumzo ya kusaka mkataba wakimataifa wa kupambana na takataka za plastiki duniani, yamemalizika hii leo mjini Geneva, Uswisi, bila ya kufikiwa makubaliano.

Baada ya miaka mitatu ya mazungumzo ambapo nchi zipatazo 180 zilikuwa zinakubaliana kwamba takataka za plastiki ni kitisho kikubwa, lakini katika mkutano huo nchi hizo bado zimetofautiana katika masuala kadhaa.

Ingawa mpaka sasa bado haijafahamika jinsi mchakato huo utakavyosonga mbele, lakini mataifa yanayozalisha mafuta yanapinga suala la ukomo wa uzalishaji plastiki zitokanazo na mafuta ya petroli, makaa ya mawe na gesi.

Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo la Ulaya, OECD, limeonya kwamba ikiwa hatua hazitochukuliwa haraka, uzalishaji wa plasitiki utaongezeka mara tatu kufikia mwaka 2060 na kuleta athari kubwa duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW