1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Geneva:kamisheni ya haki za binadam ya umoja wa mataifa yakutana

14 Machi 2005

Kamisheni ya umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya haki za binadam inaanza mkutano wake hii leo mjini Geneva.Mkutano huo wa wiki kadhaa utajadili miongoni mwa mengineyo,visa vya ukatili vinavyoendelea katika jimbo la mashariki la Sudan-Darfour.Wajumbe kutoka mataifa 53 watazungumzia pia hali namna ilivyo nchini Cuba na katika jamhuri ya Umma wa China.Marekani nayo pia itakosolewa kutokana na kashfa za mateso na wafungwa kudhalilishwa nchini Iraq na Afghanistan.Mbali na hayo wajumbe watajadiliana namna ya kulifanyia mageuzi shirika hilo la umoja wa mataifa la haki za binaadam.Mashirika yasiyomilikiwa na serikali NGO’S yamekua yakilikosoa shirika hilo .

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW