1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Mkataba wa Schengen wakubalika

6 Juni 2005

Umoja wa Ulaya na serikali ya Uswissi zimeyakaribisha matokeo ya kura ya maoni ambayo yameifanya nchi hiyo kujongea hatua moja karibu na Umoja huo.

Wananchi wa Uswissi walipiga kura ya kuunga mkono kupigwa marufuku kwa sheria za mipakani kufikia mwaka 2007 katika mkataba wa Schengen ambao unayajumuisha mataifa 13 ya Umoja wa Ulaya,pamoja na Ice land na Norway.

Uswissi si mwanachama wa Umoja wa Ulaya na mpaka sasa imekuwa ikilinda hadhi yake yakutofungamana na kambi yoyote barani Ulaya.

Katika kura nyingine ya maoni wapiga kura wameidhinisha sheria ya kuwaruhusu watu wa jinsia moja kuandikisha uhusiano wao,na kuwapa haki sawa kama za watu waliooana katika masuala yanayohusu fedha kama vile ushuru,malipo baada ya kustaafu na urathi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW