GENEVA.Tume ya haki za binadamu inataka kikao maalum kifanyike
30 Novemba 2006Matangazo
Ujerumani, Ufaransa na Kanada zinataka tume ya umoja wa mataifa ya kutetea haki za binadamu ifanye kikao maalum kitakacho jadili mzozo wa jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.
Balozi wa Ujerumani mjini Geneva Michael Steiner amesema hali ya jimbo la Darfur inazidi kuzorota na ameutaka umoja wa matifa kuchukua hatua.
Nchi 13 zaidi zilizo wanachama wa kamati ya haki za binadamu zinahitajika kuunga mkono pendekezo la kufanyika kikao hicho maalum.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan anapendelea kikao hicho maalum kifanyike amesema sifa ya kamati hiyo iko hatarini.