1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahalifu wavamia makumbusho ya kaburi la Lumumba DRC

19 Novemba 2024

Genge la wahuni limevamia makumbusho ya kaburi lilipozikwa jino la shujaa wa uhuru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Patrice Lumumba.

DRK Patrice Lumumba Tshumbe
Wanajeshi wakiwa na picha ya kiongozi wa uhuru wa Kongo aliyeuawa Patrice Lumumba wakiwa katika msafara na jeneza lake baada ya kuwasili Tshombe nchini DR Kongo Juni 22, 2022.Picha: Junior Kannah/AFP

Wizara ya utamaduni nchini humo imesema leo kuwa uvamizi  huo ulifanywa Jumatatu na kukiita kitendo hicho kuwa ni cha kikatili kilichokusudia kuharibu eneo hilo la makaburi. Jino la Patrice Lumumba ndiyo sehemu pekee ya mabaki ya waziri huyo mkuu wa kwanza wa Kongo inayohifadhiwa katika makumbusho hayo. Waziri wa utamaduni wa Kongo Yolande Elebe ameshindwa kuthibitisha ikiwa jino hilo limeporwa ama la, katika tukio hilo la Jumatatu. Lumumba aliuwawa mwaka 1961 katika mkoa wa Katanga. Mwili wake uliharibiwa kwa tindikali lakini afisa wa polisi wa Ubelgiji aliyehusika katika mauaji yake alilihifadhi jino lake kama alama ya ushindi. Jino hilo lilichukuliwa na mamlaka za Ubelgiji mnamo mwaka 2016 na kurejeshwa Kongo mwaka 2022 na kuwekwa chini ya ulinzi mkali katika makumbusho hayo chini ya mnara ambao ni alama ya mji mkuu Kinshasa.