1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Genge lauwa 47 Haiti

25 Agosti 2026

Takribani watu 47 wameuawa na wengine 22 kujeruhiwa baada ya magenge ya watu wenye silaha kushambulia eneo la Kenscoff karibu na mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, usiku wa kuamkia jana, Jumatatu.

Haiti Kenscoff 2026 | Port-au-Prince
Wakaazi wa Kenscoff wakikimbia machafuko yaliyouwa watu zaidi ya 40.Picha: Patrice Noel/REUTERS

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka huku tathmini ikiendelea.

Eneo la Kenscoff limekuwa likikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya magenge tangu mwaka jana, hali iliyowalazimu maelfu ya raia kuyahama makaazi yao.

Raia wanailaumu serikali na polisi kwa kushindwa kuzuia mauaji hayo, wakisema baadhi ya watu waliuawa karibu na kituo cha polisi bila kupata ulinzi wa kutosha.

Serikali ya Haiti imeelezea tukio hilo kuwa la kinyama na kuahidi kuimarisha usalama.

Hata hivyo, ongezeko la machafuko linaibua khofu kuhusu uwezo wa nchi hiyo kufanya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba, ambao utakuwa wa kwanza katika kipindi cha miaka kumi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW