1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Georgia yaachana na sheria yenye utata

10 Machi 2023

Bunge la Georgia leo limepiga kura kuachana na mipango ya kupitisha muswada wenye utata wa kile kinachoitwa ''sheria ya mawakala wa kigeni'', ambao ulisababisha mzozo mkubwa wa kisiasa.

Georgien | Proteste in Tiflis gegen "Agenten-Gesetz"
Picha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance

Muswada huo ulipigiwa kura wa kuondolewa baada ya kusomwa kwa mara ya pili, baada ya mbunge mmoja kati ya wabunge 36 waliopiga kura kuunga mkono sheria hiyo ambayo wakosoaji wanailinganisha na sheria za Urusi ambapo mamlaka imekuwa ikiwanyamazisha wapinzani wa Ikulu ya Urusi, Kremlin.

Mamia ya  waandamanaji wanaoipinda serikali walikusanyika nje ya majengo ya bunge wakati kura hiyo inapigwa. Viongozi wa Georgia wamekosolewa vikali kimataifa kutokana na kudhoofika kwa demokrasia na kuharibu uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW