1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Georgia yafanya uchaguzi wa bunge

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Raia wa Georgia wanapiga kura leo Jumamosi (26.10.2024) katika uchaguzi ambao utaamua uhusiano wa baadaye wa nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Georgia Irakli Kobakhidze akipiga kura mnamo Oktoba 26, 2024 huko Tbilisi, Georgia
Waziri Mkuu wa Georgia Irakli Kobakhidze akipiga kura mnamo Oktoba 26, 2024 huko Tbilisi, GeorgiaPicha: Diego Fedele/Getty Images

Takriban wapiga kura milioni 3.5 wanatarajiwa kupiga kura zao, kwa kuwachangua wabunge 150 katika Bunge la Georgia. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi mbili usiku, na matokeo yanatarajiwa mara tu baada ya uchaguzi kumalizika.

Chama tawala cha Georgian Dream kinaunga mkono ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na Urusi, wakati upinzani unaounga mkono Magharibi unataka kuchukua madaraka ili kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Georgia inataka kuwa mwanachama wa EU, lakini mchakato huo umesitishwa kwa sasa kwa sababu ya sheria tata zilizoletwa na utawala wa hivi sasa.