1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Georgia's new leaders win backing from Washington

Shaaban M Shangama24 Novemba 2003
Utangulizi: Viongozi wapya wa Georgia wameungwa mkono na Marekani, na wamesema hii leo watajitafutia msaada wa fedha wa dharura duniani baada ya kupigwa kumbo Eduard Shevardnadse katika mapanduzi yasiyomwaga damu. Washington imemuunga mkono rais wa mpito, spika wa zamani Nino Burdzhanadze, ili kuhimizha uchaguzi mpya katika jamhuri hiyo ya zamani masiki ya Kisoviet, baada ya Shevardnardze kuinamia malalamiko ya umma kuhusu hadaa uchaguzini na kujizulu. Zaidi anasimulia Shaaban Mohamed. "Marekani na jumuia ya kimataifa itayari kuisaidia serikali mpya kutayarisha chaguzi huru na za haki za bunge katika siku za usoni," alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje Richard Boucher, akaongeza kwamba waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Colin Powell alimpigia simu Burdzhanadze kwa toleo hilo la usaidizi. Powell alizungbumuza pia na Shevardnadez, na Boucher alimsifu waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Urusi - shujaa machoni mwa mataifa ya magharibi aliposaidia kukomesha vita baridi - kwa kujiuzulu baada ya miaka 11 madarakani " kwa maslahi bora kabisa ya wakazi wa Georgia".

Burdzhanadze aliwataka Wageorgia wajitahidi kurejesha nidhamu upesi iwezekanavyo, katika nchi hiyo ya milimani kwenye eneo la Caucasus, ambayo inaangaliwa kwa wasiwasi katika ulimwengu wa magharibi, kwa sababu linajengwa bomba katika ardhi yake ili kusafirisha mafuta ya Caspian hadi bahari ya Kati.

"Kuanzia kesho nidhamu na utulivu zitarejeshwa nchini na ninazitaka wakala zote za sheria zirejee katika kazi za hali ya kawaida. Na ninawaomba raia wetu wawasaidie," Burdzhanadze alisema katika hotuba yake ya televisheni hiyo jana. "Kuanzia jumatatu tutaanza mashauriano na serikali za kigeni, kuhusu msaada rasmi wa fedha na kiufundi ili kutanzua matatizo yaliytokea katika serikali iliyopita," Zurab Zhavania, kiongozi mpinzani wa ngazi ya juu, aliwaambia waandishi habari. Brdzhanandze alijumuika na kiongozi wa upinzani, Mikhail Saakashvili, kulalamika upya juu ya dai la kughilibiwa uchaguzi, katika nyendo za kuondoshwa rais madarakani katika nchi hiyo ya wakazi milioni tano.

"Hivi sasa tuko katika kipindi cha mpito," alisema Saakashvili, wakili aliyesomea Marekani akiwa na umri wa miaka 35, ambaye anatazamiwa kuwa raisa mpya. "Tunataraji kipindi cha mpito kitamalizika upesi na uchaguzi utafanywa kwa wakati," alisema. Saakashvili alieleza tuko la kuangushwa Shevardnadze kama "mapinduzi ya mahameli", akikumbusha kutolewa madarakani utawala wa kikomunisti kwa amani nchini Czechoslovakia mwaka 1989. Uchaguzi wa rais umewajibika kufanyika mnamo kipindi cha siku 45 kwa mujibu wa katiba, lakini hali ya bunge jipya linalogombaniwa inababaisha. Burdzhanadze atakuwa rais wa mpito kwa muda wa siku 45. Maelfu ya Wageorgia walishereka hadi sasa za usiku katika mji mkuu Tbilisi baada ya kumtimua Shevardnadze ofisini mwake, kwa mashtaka ya kufanya hadaa katika uchaguzi wa bunge tarehe pili mwezi huu, ambao washindi walikuwa wafuasi wake. Wakicheza ngoma, kupiga miuzi, kuimba na kupunga mikono katika magari na hata treka, walizigeuza wiki tatu za maandamano yaliyozistusha nchi jirani na serikali za magharibi kuwa pati kubwa kabisa majiani.

Watu wengi walitaraji kuanza upya katika nchi hiyo ambako mishahara ya wastani ya watumishi wa serikali ni Dolla 20. Wageorgia walishuhudia vita vya kiraia vya umwagaji damu mwanzoni mwa miaka ya tisini na mikoa miwili ilijitenga na serikali kuu. "Ninahisi kama nimezaliwa upya," Gela Papunashvili alisema katika uwanja wa bunge mjini Tbilisi, alipowakumbania na kuwabusu wageni waliomzunguka. Jumamosi, waandamanaji walilikumba jengo labunge. Kama vile ilivyotokea pale nguvu za umma zilipovuma mashariki mwa Ulaya mwaka 1989, mara hii pia wanajeshi walijiweka kando. Shevardnadze, mkuu wa chama cha Kikomunisti nchini Georgia aliacha madaraka yake, baada ya siku iliyoshuhudia ingia toka ya waziri wa mambo ya nje wa Russia Igor Ivanov baina ya kiongozi huyo mkongwe na kambi ya upinzani. Russia ilisema inaangalia kwa makini matokeo ya Georgia, nchi ambayo inapokea gesi na nishati rahisi kutoka kwa mtawala wake wa zamani. Msemaji wa Kansela Gerhard Schroeder alisema kwamba Eduard Shevardnadze anakaribishwa akitaka kuja Ujerumani." Iwapo Eduard Shevardnadeze anataka kuja Ujerumani, basi anakaribishwa kutokana na msaada wake katika juhudi za kuungana upya Ujerumani," Bela Anda aliliambia shirika la habari la Reuters.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW