Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius yupo Ukraine
21 Novemba 2023Matangazo
Ni ziara ya pili ya Pistorius mjini Kyiv na inajiri siku moja baada ya ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.Kyiv imekuwa na wasiwasi kuwa vita vya Mashariki ya kati vingesababisha kupungua kwa msaada kutoka kwa washirika wake. Ujerumani ambayo ni mfadhili mkuu wa pili wa msaada wa kijeshi kwa Ukraine baada ya Marekani, inalenga kuondoa hofu hiyo ya Ukraine.Pistorius anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati huu Urusi ikizidisha mashambulizi yake nchini humo. Watu watatu wameuawa kufutia mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo katika mikoa ya mashariki mwa Ukraine ya Kharkiv na Donetsk.