1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annalena Baerbock ametoa wito kulindwa Ukanda wa Gaza

21 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua jukumu la kulinda raia katika Ukanda wa Gaza baada ya mzozo wa sasa kati ya Israel na kundi la Hamas kukamilika.

Berlin, Deutschland | Annalena Baerbock im Interview mit Jaafar Abdul Karim
Picha: Ronka Oberhammer/DW

Akizungumza na mwandishi wa DW Jaafar Abdul-Karim, Baerbock amehimiza jamii ya kimataifa kufanya juhudi zaidi kupunguza mzozo kwa sasa. Aidha ametetea msimamo wa Ujerumani wa kuhimiza usitishwa wa vita kwa muda mrefu, na kusisitiza kuwa kipaumbele kwa wakati huu kinapaswa kupeleka misaada ya kibinadamu kwa wakaazi wa Gaza.Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani ameeleza kuwa, pindi tu mzozo wa sasa utakapokamilika, jamii ya kimataifa inapaswa kuhakikisha hali ya utulivu inarudi katika ukanda wa Gaza ndani ya muktadha wa suluhisho la mataifa mawili kwenye mzozo wa Israel na Palestina. Ameiambia DW kuwa, "ili kuhakikisha usalama, tunahitaji uwajibikaji wa kimataifa." Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani ameitembelea Israel mara tatu tangu mzozo ulipozuka mnamo Oktoba 7 wakati wanamgambo wa Hamas walipofanya shambulizi ndani ya ardhi ya Israel na kuua watu 1,200 na kuwachukua mateka watu 240.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW