1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSierra Leone

Ghala la silaha la kijeshi la Sierra Leone lashambuliwa

26 Novemba 2023

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS leo imelaani jaribio la baadhi ya watu la kuchukuwa silaha na kuvuruga utaratibu wa kikatiba nchini Sierra Leone

Wanajeshi wa Sierra Leone baada ya kuchukuwa tena udhibiti wa mji wa Masiaka mnamo Mei 13, 2000
Wanajeshi wa Sierra LeonePicha: Issouf Sanogo/AFP

Serikali ya Sierra Leoned imeripoti leo kuwa ghala lake la silaha za kijeshi limeshambuliwa katika mji mkuu wa Freetown.

Kufuatia tukio hilo, serikali hiyo imetangaza mara moja amri ya kitaifa ya kutotoka nje. Aidha taarifa zinasema kuwa vikosi vya usalama vimefanikiwa kudhibiti hali hiyo.

Soma pia:Upinzani waapa kutoshiriki katika uongozi Sierra Leone

Hali ya kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi imesalia kuwa ya wasiwasi tangu kuchaguliwa tena kwa Rais Julius Maada Bio katika uchaguzi uliopingwa na mgombea mkuu wa upinzani mnamo mwezi Juni

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW