UhalifuAfrika
Ghala la WFP laporwa na waasi wa RSF nchini Sudan
29 Desemba 2023Matangazo
Shirika hilo limeeleza kuwa bidhaa zilizoibiwa wikiendi iliyopita huko al-Jazirah ikiwa ni pamoja na nafaka, mafuta na mboga za majani zingeliweza kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni wapatao 1.5.
WFP imesema kuwa vikosi vya RSF vimepora pia lishe maalum 20,000ambazo kwa kawaida hutolewa kwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo pamoja na wanawake wanaonyonyesha.
Soma pia:Kiongozi wa kundi la RSF la Sudan atembelea Uganda na kukutana na Rais Museveni
Kundi la RSF linaloongozwa na Mohamed Dagalo limekuwa likipambana na jeshi la Sudan tangu mwezi April mwaka huu (2023).