1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghana huenda ikashindwa, fainali ya Kombe la Mataifa Afrika

12 Novemba 2024

Mabingwa mara nne wa Kombe la Mataifa ya Afrika Ghana wanaweza kushindwa kufuzu fainali ya michuano hiyo katika mechi mbili zilizosalia.

Kombe la Mataifa ya Afrika
Ghana huenda ikashindwa kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa AfrikaPicha: Ulrik Pedersen/DeFodi Images/picture alliance

Ni Misri tu na Ivory Coast ambazo zimetinga fainali za michuano hiyo mara nyingi kuliko Black Stars lakini huenda Ghana wakawa nje ya orodha ya timu zitakazofuzu kufikia Alhamisi. 

Washindi wawili wa juu katika kila moja ya makundi 12 watafuzu kwa fainali za mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.

Mechi za mzunguko za kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON zinaendelea

Ghana wanashika nafasi ya tatu katika Kundi F wakiwa na pointi mbili katika mechi nne, huku Angola wakiwa tayari wamefuzu na Sudan wakihitaji sare tu katika michezo miwili ili kuungana na Angola.

Angola imeweka rekodi ya asilimia 100 wakiwa na ushindi mara nne mfululizo huku Sudan wakiwa na alama saba na watamenyana na Niger walio mkiani. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW