1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGhana

Ghana kuzingatia nidhamu kuhusu mkopo wa IMF

24 Mei 2023

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, amesema Jumanne kwamba serikali yake inapanga kuzingatia mbinu za kinidhamu katika kutekeleza mpango wa mkopo wa Shirika la Fedha Duniani, IMF.

ECOWAS Westafrikanische Staaten verhängen Sanktionen gegen Mali und Guinea
Picha: Nipah Dennis/AFP

Wiki iliyopita, bodi kuu ya IMF iliidhinisha mkopo wa dola bilioni tatu kwa miaka mitatu kwenye taifa hilo la Afrika, na kulipwa mara moja kiasi cha dola milioni 600.

Akufo-Addo ameliambia jukwaa la kiuchumi la Qatar lililoandaliwa na Bloomberg kwamba Ghana imejizatiti kurekebisha matumizi na mpango wa IMF utairuhusu serikali yake kupata masoko ya madeni ya kimataifa.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kubadilisha dhahabu kwa mafuta, rais huyo wa Ghana amesema hilo linafanyika tayari, na linasaidia.

Ghana na Ivory Coast wazalishaji wakuu wa kakao duniani, zimekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwenye mataifa ya Magharibi, ikiwemo Umoja wa Ulaya kutokana na kuhusika na ajira ya watoto katika mashamba ya kakao.