1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghana yaahidi kutamba katika Kombe la dunia Ujerumani

Ramadhan Ali22 Mei 2006

Ghana itakata kiu cha miaka 44 kutocheza katika Kombe la dunia na inaahidi kutamba.Ujerumani imepiga kambi Uswisi na El Guerrouj kustaafu katika riadha.

Wachezaji wa timu ya Ghana
Wachezaji wa timu ya GhanaPicha: FAG

Tukianza na maandalio ya Kombe la dunia,kocha wa Ujerumani, Jürgen Klinsmann mwishoe, aliweza jana kukusanya pamoja kikosi chake chote cha wachezaji 23 huko Uswisi.Wa mwisho kuwasili alikuwa Jens Lehmann baada ya kulinda kati ya wiki iliopita lango la Arsenal katika finali ya Kombe la ulaya la klabu bingwa-champions League dhidi ya FC Barcelona ya Spain.Hakuwapo huko Sardinia,Itali ambako timu ya Ujerumani ilipitisha likizo fupi.

Beki wa shoto wa Ujerumani alieumia Philipp Lahm, alijiunga na kikosi hicho huko Sardinia,lakini siku ya mwisho tu baada ya opreshini aliofanyiwa kwenye kisugudi chake.

Timu ya Taifa ya Ujerumani itabakia Geneva,Uswisi kwa mazowezi hadi mei 30.Itavuka mpaka kwa safari fupi kuingia freiburg kucheza na Luxembourg hapo mei 27.Halafu Mei 30,Ujerumani ina miadi ya kupimana nguvu na Japan mjini Leverkusen na Colombia Juni 2 mjini Moenchengladbach kabla kurejea ngamani Berlin,maskani yake kwa Kombe hili la dunia.

Katika kambi ya Uingereza,mshambulizi wao Wayne Rooney aonesha aweza kuwa fit kuichezea Uingereza juni hii katika Kombe la dunia-hii ni kwa muujibu wa daktari wa timu ya Uingereza aliefurahishwa na jinsi chipukizi huyo anavyopata nafuu haraka.Rooney aliumia na kuvunjika guu wakati wa changamoto kati ya klabu yake ya Manchester Unite dna Chelsea.Chelsea iliikomea MANU mabao 3:0.

Uingereza ina miadi Juni 10 kufungua dimba lake la Kombe la dunia na Paraguay.Rooney ndio minga mkubwa wa m anulari ya Uingereza katika Kombe hili la dunia.

Beki mshahara wa Uingereza na Arsenal london, Sol Campbell,yadhihirika atahamia klabu ya Fernerbahce ya Uturuki.Gazeti la Daily Mirror na Daily Star yote yameripoti kuwa, klabu hiyo ya uturuki imejitolea kulipa dala milioni 15 kwa beki huyo mshahara kwa mkataba wa miaka 3.Campbell ndie alietia bao la Arsenal katika changamoto ya wiki iliopita ya kuania Kombe la klabu bingwa barani ulaya na FC Barcelona.

Ghana au Black Stars inaahidi kukata kiu cha miaka 44 cha kutocheza katika Kombe la dunia kwa kuwafurahisha mashabiki sio tu wa nyumbani bali Africa nzima.

Mojawapo ya timu kali kabisa barani Africa kwa miaka mingi,iliotoa mastadi kama Abedi Pele,Anthony Yeboah,Samy Koufour na sasa Michael Essien,haikuwahi kucheza katika Kombe la dunia ingawa ndio mabingwa mara 4 wa Afrika.

Kocha wa Ghana kutoka Serbia,Ratomir Dujkovic,amesifiwa sana kwa kuikatia tiketi Ghana katika Kombe hili la dunia 2006.Isitoshe,shirikisho la dimba la Ghana ambalo mara nyingi ni halina fedha, mara hii limeimarika kwa kuwa na wafadhili wengi.Hii imeiwezesha Ghana kuwaita ma stadi wake waliotawanyika kila pembe ya Ulaya.

Majogoo wake 2-Essien na Ali Muntari walikosa kucheza katika kombe la Afrika la mataifa huko Misri mapema mwaka huu kutokana na kuumia na hi indio pengine iliosababisha Ghana kupigwa kumbo na mapema.Hapa Ujerumani, Black Stars wanaahidi mambo yatakua vyengine Juni hii.

Pamoja na nahodha wao Steven Appiah,Ghana inaahidi makubwa katika Kombe hili la dunia ili kurejesha hadhi yake kuwa ndio ‘Brazil ya Afrika’.

Kinyan’ganyiro cha Kombe la Afrika mashariki na kati kinarejea kesho uwanjani huko Tanzania baada ya baadhi ya timu pamoja na polisi ya Zanzibar kuaga mashindano na moja kujazwa kikapu chake mabao 19 .

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la COSAFA-kusini mwa Afrika-Castle Cup,Botswana kwa msangao imeipiga kumbo jana Bafana Bafana-Afrika Kusini kufuatia changamoto ya mikwaju ya penalty ya 6-5.

Hapo jumamosi Botswana ilizaba Madagaskar 2:0 na Afrika kusini ikaitoa Swaziland kwa bao 1:0.sasa Botswana inajiunga na washindi wa kundi A- Angola na mabingwa Zimbabwe katika nusu-finali ya castle Cup.Burundi inahangaikia kupata mfumo bora wa Ligi yake ya timu zaidi ya 50 kama anavyosimulia Nimobouna Abdullah kutoka Bujumbura.

Bingwa mara 2 wa olimpik Hicham el Guerrouj wa Moroko anatazamiwa kustaafu.Kwa muujibu wa duru karibu nae,El Guerrouj,bingwa wa mita 1500 na mita 5000 anatazamiwa kutangaza leo kustaafu.Akiwa na umri wa miaka 31, El Guerrouj,aliwasangaza mashabiki alipotimika mbio katika michezo iliopita ya olimpik huko Athens,Ugiriki mwaka jana na kutwa MEDALI ZA dhahabu katika mita 1.500 na mita 5000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW