1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghana yafufua matumaini, Bafana bafana bado iko hai

24 Januari 2015

Baada ya kuugua malaria mshambuliaji Asamoah Gyan wa Ghana amerejea dimbani katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika na kufunga bao la ushindi dhidi ya Algeria inayopigiwa upatu kutoroka na taji hilo.

Afrikan Cup 2015 Ghana vs. Algerien 23.01.2015
Asamoah Gyan akimtoka mlinzi wa Algeria na kupachika bao la ushindiPicha: Getty Images/AFP/C. de Souza

Senegal lakini imekuwa kinara wa kundi C baada ya kupambana kutoka nyuma na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Afrika kusini.

Kundi hilo bado halina mwenyewe baada ya goli la Gyan mwishoni kabisa wa mchezo huo dhidi ya Algeria katika uwanja wa mjini Mongomo, ambapo Ghana sasa iko sawa kwa pointi na Algeria zote zikiwa na pointi tatu baada ya michezo miwili, pointi moja nyuma ya Senegal.

Mshambuliaji wa Ghana Mubarak wakaso(L) akipambana na Sofiane Feghouli wa AlgeriaPicha: Reuters/Mike Hutchings

Afrika kusini kibarua kigumu

Afrika kusini ina kazi ngumu sana kuweza kufikia robo fainali , ikiwa na pointi moja tu kibindoni, lakini hata Bafana bafana hawajayaaga mashindano kabla ya mchezo wa mwisho.

Kundi la C limekuwa kama lilivyotarajiwa kuwa ni kundi gumu la kifo na imekuwa hivyo zaidi baada ya Asamoah Gyan kukimbilia mpira mrefu kutoka nyuma na kutandika mkwaju wa moja kwa moja na kuipa matumaini timu yake ya kusonga mbele katika robo fainali, wakati ikiiweka Algeria katika kibarua kigumu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Senegal.

Kikosi cha timu ya taifa ya Afrika kusini, Bafana bafanaPicha: P. Utomi Epkei/AFP/Getty Images

"Wakati tukiingia katika michezo ya mzunguko wa mwisho, timu kubwa haitaingia katika duru ijayo," amesema kocha wa Senegal Alain Giresse.

Kikosi cha Giresse kiko katika nafasi nzuri kikihitaji sare tu kufikia robo fainali baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Afrika kusini Bafana bafana na kuwa timu pekee katika kundi hilo ambayo haijashindwa.

Gharama ya kutafuta sare

Gyan ni mchezaji muhimu kwa Ghana lakini alikosa mchezo wa kwanza kutokana na homa ya malaria na alibidi kulazwa katika hospitali mjini Mongomo.

Algeria iligharamika kutokana na kutoweka msukumo zaidi katika ushindi dhidi ya Ghana na kuridhika kupata sare. "Vijana hawakucheza kwa kufuata maelekezo," kocha wa Algeria Christian Gourcuff amesema, na pia akadai timu yake haikusaidiwa na kile alichosema kuwa ni uwanja mbovu mjini Mongomo na hali ya joto katika mji huo wa mashariki mwa Guinea ya Ikweta.

Kikosi cha timu ya taifa ya AlgeriaPicha: imago

Pamoja na hayo mashindano haya yanayofanyika nchini Guinea ya Ikweta mbali ya matatizo kadhaa lakini yameonbesha mafanikio makubwa hadi sasa. Tunisia ilibidi kuoga katika bwawa la kuogelea katika hoteli yao na Ghana walilalamika safari ndege za basi kwenda katika mazowezi, lakini wiki ya kwanza ya kombe la mataifa ya Afrika ambalo lilitarajiwa kuvurugika linaweza kuonekana kuwa ushindi miubwa hadi sasa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre /ape

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW