Ghana yapunguza vifo vya watoto
11 Mei 2012Hosipitali ya La Genera ACCRA-Ghana ambacho ni kituo cha kwanza kutoa chanjo. Wanaonekana akina mama wakiwa na watoto wao migongoni wakijongea kupata chanjo katika foleni maalumu kila mmoja wao anaiheshimu foleni inayowapa nafasi ya kupata matone ya chanjo.
Mandhari ya eneo hilo ikipambwa na kilio cha mtoto akijua kuwa sasa anaenda kudungwa sindano kumbe anafuata matone ya chanjo.
Wakipatiwa msaada na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia watoto, UNICEF, kwa sasa kati ya watoto wadogo chini ya miaka mitano 1000 watoto 80 wanaofariki chini ya umiri huo wakati kwenye mataifa mengine barani humo hali inatisha, mfano katika Somalia kati ya watoto 1000 watoto180 wanafariki kabla ya kufiki umri wa miaka mitano.
Mafanikio yakiwa makubwa kwa mataifa ya Ulaya, Sweden na Finland kati ya watoto1000 ni watoto watatu tu ndiyo wanaofariki chini ya umri huo.
Ghana imeshauriwa kupunguza kabisa vifo vya watoto kutoka 80 hadi 40. Kwa sasa chanjo wanazopatiwa watoto hao ni pamoja na Virusi vya Rota na Pneumococcal kwa ajili ya homa ya mapafu.
Wakati chanjo zikiendelea kutolewa asimilia 87 ya chanjo za Polio, Kifua Kikuu, Pepopunda, Homa ya manjano na chanjo nyingine za watoto zimetolewa.
Akiwa kazini, mhudumu wa afya ndani ya nyumba moja akitoa chanjo, hapa anataja umuhimu wa chanjo ya polio.
"Chanjo ya polio tunawapa watoto kujikinga na ugonjwa huu ambapo wakipata ugonjwa huo hatari mwili unapoooza, ila ukimpa chanjo mapema inazuia kabisa kuambukizwa ugonjwa huo." anasema mhudumu wa Afya.
Chanjo hizo wanapewa watoto kabla ya kufikia miezi minne ambapo vituo vya Afya kadhaa vimepewa chanjo, wengine wakizunguka majumbani kuhakikisha watoto wote wanafikiwa na mpango huo, lakini changamoto kubwa ni kuzishawishi baadhi ya kaya ambazo wanaamini kuwa kumpa chanjo mtoto kuna madhara hasa wale wanaoamini katika ushirikina.
Taasisi ya muunganiko wa GAVI imefanikisha kuwafikia watoto 400,000 katika taifa hili lenye watu milioni 25. Huku chanjo hizo zinategemea kupunguza vifo vya homa ya manjano kwa watoto 12,000, kuhara kwa watoto 10,000 wakilenga kufikia malengo ya milenia mwaka 2015 sasa wako katika hatua nzuri.
Changamoto nyingine ni vifo vinayotokana na Malaria na Utapia mlo; hii linanonekana wazi kuwa utapia mlo mara nyingi umekuwa ukiongeza idadi vya vifo vya watoto hao.
Sasa kila mwanamke mjamzoto wa Ghana anaona umuhimu wa kupatiwa chanjo kwa watoto wake. "Nikijifungua mtoto wangu salama nitampeleka kupata chanjo." alisema mwanamke mjamzito.
Akinamama wanaojifungua wameshauriwa kuwanyonyesha watoto wao kwa miezi sita ya mwanzo kwa kuwapa maziwa ya mama tu. Huku kukiwa na ushahidi kuwa akina mama wengi hawafanyi hivyo kwa kutoona umuhimu wa kunyonyesha watoto na wengine wakibanwa na majukumu ya kazi katika sekta mbalimbali.
Mwandishi:Adeladius Makwega
Mhariri: Miraji Othman