SiasaGhana
Ghana yatangaza Waafrika kuingia bila visa
3 Januari 2025Matangazo
Hatua hiyo ni kuelekea katika ushirikiano wa kiuchumi wa bara hilo. Hilo limetangazwa katika hotuba yake ya mwisho wakati akijiandaa kuachia madaraka Januari 6, baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
Akilihutubia bunge, Akufo-Addo amesema anajivunia kuidhinisha hatua hiyo kwa wale wote wenye pasi za kusafiria za Afrika.
Amesema hiyo ni hatua ya kimantiki inayofuata katika Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika, AfCFTA.
Kwa mujibu wa Akufo-Addo hayo yote ni mambo muhimu katika utekelezaji wa Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, ambayo inatazamia kuwa na Afrika iliyounganishwa ifikapo 2063.
Ghana inaungana na Rwanda, Ushelisheli, Gambia na Benin kuwaruhusu wasafiri wenye pasi za Afrika kuingia kwenye nchi hizo bila visa.