Ghana:Kuanza uzalishaji chanjo ya Covid
30 Machi 2022Taasisi ya Kitaifa ya Chanjo itaanzishwa ili kuweka wazi mkakati kwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuanza awamu ya kwanza ya uzalishaji wa sindano kwa ajili ya kuziuza, alisema Rais Nana bila kutoa maelezo zaidi.
"Muswada utaletwa kwenu, katika bunge hili ili kupata idhini ya kuanzishwa kwa taasisi ya kitaifa ya chanjo" Alisema.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters hadi sasa Ghana imechanja kikamilifu 21.5% kati ya wakaazi wake milioni 30.
Soma zaidi:Ujumbe wa ECOWAS kukutana na waliopindua serikali Guinea
Wiki iliyopita serikali ya nchi hiyo iliondoa vikwazo vya virusi vya Corona kutokana na kile ilichokitaja kupungua kwa kasi ya maambukizi na kampeni kabambe ilizofanya katika kukabilianana janga hilo ambalo linaendelea kuikabili dunia.
Kuanza kazi kwa kiwanda kipya cha magari Ghana
Kadhalika rais huyo alitangaza kuanzishwa kwa kiwanda kipya cha utengenezwaji wa magari kilichoanzishwa na kampuni ya Nissan, katika mji wa bandari wa mashariki wa Tema kitakachokuwa na uwezo wa kutengeneza magari mapya 5,000 kwa mwaka.
Soma zaidi:Akufo-Addo wa Ghana aapishwa kwa muhula mwingine madarakani
Kwa sasa kampuni hiyo inazalisha magari aina ya Nissan na Peugeot kwa ajili ya soko la Ghana na Afrika Magharibi.
Rais Nana alaani vikali mapinduzi ya kijeshi kwa majirani zake
Katika hotuba yake kwa bunge la kitaifa Rais Nana ameoneshwa kuchukizwa kufuatia mfufululizo wa mampinduzi ya kijeshi ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika ukanda wa Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel na hatua iliosababisha mataifa hayo kukabiliwa na vikwazo kadhaa kutoka jumuia mbalimbali ikiwemo jumuia ya kiuchumi Afrika Magharibi ECOWAS
Alisema katika kipindi cha miezi 18 iliopita eneo hilo la Afrika Magharibi lilitengeneza vichwa vya habari katika vyombo vya habari vya kimataifa kutokaa na kile alichokiita "sababu zote zisizo sahihi."
Soma zaidi:ECOWAS kutoiwekea vikwazo Burkina Faso
Alisema serikali za Burkina Faso, Guinea na Mali zilizo na kila kitu zimepinduliwa tangu Agosti 2020, na viongozi wa kikanda wanatafuta kuharakisha kurejea kwautawala wa kikatiba kwa kuweka vikwazo na kauli za mwisho.
"Hatutamani kuwa kisiwa cha amani na utulivu eneo la machafuko," alisema Akufo-Addo, ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuia ya kikanda ya Afrika Magharibi ECOWAS.
Chanzo:Reuters