1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia za soka Misri

26 Machi 2012

Mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa huku wengine 18 wakijeruhiwa wakati mashabiki wa soka waliojawa na hasira walipopambana na polisi katika mji wa Port Said nchini Misri

FILE - In this Wednesday, Feb. 1, 2012 file photo, Egyptian fans clash with riot police following the Al-Ahly club soccer match against the Al-Masry club at the soccer stadium in Port Said, Egypt. Egypt's top prosecutor has charged 75 people with murder and negligence in connection with a deadly soccer riot last month in the Mediterranean city of Port Said. (AP Photo, File).
Ägypten Fußballspiel AusschreitungenPicha: AP

Shirikisho la soka la Misri EFA limeifungia klabu ya al-Masry, kucheza misimu miwili kutokana na uvamizi wa mashabiki wake uliofanywa uwanjani na kuwauwa watu 74 mwezi uliopita, katika ghasia mbaya zaidi kufanywa nchini humo tangu maandamano yaliyomwondoa madarakani Rais Hosni Mubarak mwaka uliopita.

Shirika hilo la EFA liliamuru uwanja wa michezo wa Port Said , ambako vurugu hizo za  mashabiki zilitokea baada ya klabu ya al-Masry kuizaba Al Ahli ya Cairo, ufungwe kwa miaka mitatu.

Wachezaji wa Al Ahly wakitoroka uwanjani baada ya mashabiki wa Al Masry kuzua rabshaPicha: picture-alliance/dpa

Jeshi la polisi lilifyatua risasi hewani kuwatawanya mamia ya mashabiki wa soka waliokuwa wakiandamana nje ya jengo la Mamlaka ya Suez Canal mjini Port Said. Walioshuhudia wamesema ghasia hizo zilianza jana usiku na kuendelea hadi mapema leo.

Wakati huo huo, miamba wa soka ya Afrika Al Ahly ya Misri itacheza kesho Jumapili ugenini dhidi ya klabu ya Coffee ya Ethiopia katika mchuano wa kwanza wa tangu watu 74 kufariki mwezi uliopita baada ya ghasia kuzuka kufuatia mchuano na klabu hasimu ya al Masry.

Maafisa waliojawa uwoga walishindwa hata kuikubalia Al Ahly kucheza mechi za kirafiki kabla ya mchuano huo wa awamu ya pili, mkondo wa kwanza wa kombe la ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Cofee katika uwanja wa kitaifa wa Addis Ababa.

Vita vya Dortmund na Bayern

Katika soka ya Ujerumani, mashabiki wa soka wanaendelea kununua kwa wingi tiketi za fainali ya mwaka huu ya kombe la shirikisho Ujerumani DFB Pokal baina ya Borussia Dortmund na mahasimu wake wakuu Bayern Munich, huku kukiwa na maombi 328,000 yaliyopokewa.

Kombe la Shirikisho la Ujerumani maarufu kama DFB PokalPicha: picture alliance/augenklick

Dortmund itapambana na Bayern katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin mnamo Mei 12 huku timu hizo mbili za ligi ya Bundesliga zilikutana katika marudio ya fainali ya mwaka 2008 ambapo Bayern ilishinda magoli mawili kwa moja baada ya muda wa ziada.

Shirikisho la Soka la Ujerumani DFB limepokea zaidi ya theluthi ya maombi milioni moja yaliyotumwa kwa viti 75,000 ambavyo bado vingali na nafasi baada ya tiketi 20,000 kupewa kila klabu kuwapa mashabiki wake.

Muamba angali hospitalini

Nchini Uingereza ni kuwa kiungo wa Bolton Fabrice Muamba angali anakabiiwa na kipindi kirefu cha kupata nafuu, baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa uwanjani wiki iliyopita, licha ya hali yake kuimarika zaidi tangu alipozirai.

Chanzo cha mshtuko wa moyo wa Muamba bado hakijabainikaPicha: AP

Babake Muamba na mchumba wake walitoa taarifa jana Ijumaa wakiwashukuru mashabiki, viongozi wa soka, na madaktari kwa kuwa pamja nao tangu Muamba alipopatwa na tatizo hilo.

Muamba mwenye umri wa miaka 21 angali katika chumba mahututi cha Hospitali ya London Chest nchini Uingereza ambapo anaendelea kupata nafuu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Mohamed Dahman