1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia zaibuka maandamano ya kupinga ufisadi Mexico

16 Novemba 2025

Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa wengine 20 wakikamatwa wakati wa maandamano makubwa mjini Mexico City yaliyopinga namna Rais Claudia Sheinbaum anavyoshughulikia uhalifu.

Maandamano ya Mexico City
Muandamanji aliyeficha uso Mexico City akiwakabili polisiPicha: Ian Robles/ZUMA Press Wire/IMAGO

Maelfu ya waandamanaji waliandamana hadi eneo la Zolacalo, wakiongozwa na vijana wa Gen Z na  wafuasi wa "vuguvugu la Sombrero" lililoibuka baada ya kuuawa kwa Meya Carlos Manzo aliyekuwa mstari wa mbele kupambana na magenge ya dawa za kulevya.

Ghasia ziliibuka baada ya kundi la waandamanaji waliyoficha uso kuvunja vizuizi na kurusha mawe, polisi ilijibu kwa kuwatawanya waandamanji kwa gesi ya kutoa machozi. Polisi pia inachunguza madai ya kushambuliwa kwa mwandishi wa habari.

Waandamanaji wanamlaumu rais kwa ufisadi na kushindwa kupambana na magenge. Serikali imesema kuwa maandamano hayo yamefadhiliwa kutoka nje ya nchi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW