Israel inaendelea kupambana na mashambulizi ya Wapalestina
10 Oktoba 2015Wakati huo huo majeshi ya usalama ya Israel yanapambana kudhibiti wimbi la mashambulizi ya Wapalestina ya kuchoma visu raia na wanajeshi.
Kwa mara ya kwanza tangu ghasia hizo kuzuka, mapambano yametokea katika mkapa na ukanda wa Gaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo linalotawaliwa na kundu la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas walipoanza kusukuma matairi yaliyowashwa moto na kurusha mawe dhidi ya vikosi vya jeshi la Israel katika mpaka.
Wapalestina sita wameuwawa na wengine zaidi ya kumi na mbili wamejeruhiwa, wizara ya afya ya Palestina imesema .
Jeshi la Israel limesema "zaidi ya watu 1,000 waliokuwa wakifanya ghasia walijipenyeza katika eneo lililotengwa bila shughuli za kijeshi na kupambana na majeshi ya Israel katika uzio wa usalama. Watu waliofanya ghasia walifika katika uzio huo wa waya wa kuweka usalama , wakirusha maguruneti, mawe na matairi yaliyochomwa moto kwa wanajeshi wa Israel ...wakitishia kuvuka uzio huo na kuvamia jamii zilizoko karibu na hapo." Jeshi hilo limesema vikosi vya Israel vilifyatua risasi za tahadhari na kisha vilivyatua risasi dhidi ya watu hao kuwazuwia kusonga mbele.
Vijana wa Kipalestina na mashambulizi
Siku za hivi karibuni zimeshuhudia mashambulizi ya vijana wa Kipalestina wakiwa na vifaa vya nyumbani kama visu, vifaa vya ujenzi na hata vya kumenyea mboga na matunda. Vijana hawana mahusiano na makundi yenye silaha ambayo yamekuwa yakishambulia wanajeshi wa Israel na raia wakati wowote, na kuweka juhudi za kuleta usalama katika hali ya utata.
Ghasia hizo , ikiwa ni pamoja na shambulio la kwanza la kulipiza kisasi lililofanywa na Muisrael, linaongeza hofu ya ghasia hizo kusambaa zaidi na kutoweza kudhibitiwa.
Hali ya kutoweza kutabirika na ukatili wa mashambulio hayo, pamoja na vijana wenye umri mdogo wanaoshambulia , imewashangaza Waisrael na kuzusha hofu kwamba ghasia mpya za Wapalestina ama Intifada huenda inakaribia.
Mjini Jerusalem, Mpalestina mmoja amemchoma kisu na kumjeruhi kijana wa Kiisrael mwenye umri wa miaka 14 jana Ijumaa na baadaye alikamatwa. Katika shambulio jingine karibu na lango la Kiryat Arba, la makaazi ya Wayahudi katika ukingo wa magharibi , Mpalestina alipigwa risasi na polisi na kufariki baada ya kumshambulia kwa kisu na kujaribu kumnyang'anya silaha, polisi ya Israel imesema.
Katika upande wa kaskazini nchini Israel , mwanamke mmoja muarabu mwenye umri wa miaka 29 alipigwa risasi na kujeruhiwa wakati akijaribu kuwachoma kisu watu katika kituo cha basi katika mji wa Afula , ambako tukio jingine la kuchoma visu lilitokea siku moja kabla, polisi imesema.
Kiongozi wa Hamas katika ukanda wa Gaza Ismail Haniyeh amesifu mashambulizi ya hivi karibuni ya Wapalestina ya kuchoma visu katika maeneo ya Israel katika hotuba wakati wa sala ya Ijumaa , akiieleza hali hiyo kuwa ni intifada.
Ghasia haziko katika kiwango cha Intifada
Maafisa wa Israel wamesema ghasia hizo haziko katika kiwango hicho kwa sasa, lakini ni ghasia zinazozushwa kila mara katika miongo kadhaa.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu amezieleza ghasia hizo kuwa ni "wimbi la ugaidi."
Yeye pamoja na rais wa palestina Mahmoud Abbas wamejerabu kupunguza hali ya wasi wasi katika siku za hivi karibuni lakini wote wanaonekana kutoweza kudhibiti ghasia hizo.
Utawala wa rais Barack Obama umeshutumu ghasia hizo na mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya raia wa Israel na wanajeshi na kutoa wito wa utulivu kwa pande zote.
Mjini Washington , msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani John Kirby ameyaeleza mashambulizi yanayofanywa na Wapalestina dhidi ya Waisrael kuwa na "vitendo vya kigaidi.
Mapema jana Muisrael mmoja aliwachoma kisu na kuwajeruhi Waarabu wanne kusini mwa Israel katika shambulio linaloonekana ni la kulipiza kisasi.
Waziri mkuu wa Israel ameshutumu shambulio hilo la Muisrael kuwashambulia waabu wanne.
Benjamin Netanyahu , ameshutumu vikali kuwadhuru Waarabu wasio na hatia. Mapema mtu mmoja Muisrael aliwachoma kisu na kuwajeruhi Waarabu wawili Bedouin mjini Dimona kusini mwa nchi hiyo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / ape
Mhariri: Sudi Mnette