GHAZNI : Mateka wawili wa kike wa Korea kuachiliwa leo
13 Agosti 2007Matangazo
Wanamgambo wa kundi la Taliban wanaowashikilia mateka wafanyakazi wa misaada 21 wa Korea Kusini wamesema kwamba watawaachilia huru mateka wawili wa kike leo hii.
Gavana wa jimbo la Ghazni ambapo mateka hao wanashikiliwa ametowa tangazo hilo baada ya kuahidiwa na Taliban.Gavana huyo alikuwa akizungumza baada ya ahadi ya wanamgambo ya kuwaachilia wanawake hao wawili ambao wako mahtuti kushindwa kutimizwa hapo jana.
Wajumbe wa Taliban na Korea Kusini wamekuwa wakikutana kwa mara ya tatu kwa mazungumzo ya kuachiliwa huru kwa mateka hao 21.Wanamgambo wanasema Wakorea Kusini wataachiliwa huru iwapo tu serikali ya Afghanistan itawaachilia huru idadi kama hiyo ya wafungwa waasi dai ambalo serikali imelikataa.